RAIS wa klabu ya Barcelona, Sandro Rosell amebainisha kuwa mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Lionel Messi haendi popote kipindi chote atakachokuwa kiongozi wa klabu hiyo. Rosell amesema ingawa hawezi kusema haiwezekani lakini litakuwa jambo gumu kwa nyota huyo kuondoka hapo wakati akiwa kiongozi. Messi mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or mara nne kwasasa ni majeruhi na atakuwa nje ya uwanja mpaka Januari mwakani. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina ana mkataba na Barcelona unaomalizika 2018 wakati akitimiza miaka 31 lakini kumekuwa na tetesi kuwa kuna uwezekano wa nyota huyo kuondoka.
No comments:
Post a Comment