MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini anaamini kuwa nahodha wake Vincent Kompany atakuwa fiti kwa ajili ya mchezo dhidi ya West Bromwich utakafanyika Jumatano. Kompany amekuwa nje ya uwanja toka apate majeraha ya msuli katika mchezo dhidi ya Everton uliochezwa Octoba 5 mwaka huu. Pamoja na kufanya vizuri mechi za nyumbani, City wamekuwa wakihangaika katika mechi za ugenini za ugenini na kushinda mechi moja pekee toka msimu huu umeanza hivyo ujio wa beki huyo unaweza kuwa ahueni kwa Pellegrini. Akihojiwa Pellegrini amesema anadhani Kompany anatakuwepo katika mchezo wa ugenini Jumatano. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa mchezo huo ni muhimu kwao kushinda kama wanahitaji kuendelea kuwa katika mbio za kugombea taji la ligi.
No comments:
Post a Comment