MACHO na masikio ya mamilioni ya mashabiki wa soka Ijumaa hii yatahamia katika kiota cha Costa do Sauipe kilichopo katika jimbo la Bahia nchini Brazil kushuhudia upangwaji ratiba ya michuano ya Kombe la Dunia 2014. Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limetenga kiasi cha dola milioni nane kwa ajili ya shughuli hiyo itakayoonyeshwa dunia nzima kwa dakika 90 huku ikishirikisha nyota wa soka wa Brazil pamoja na muziki utakaowapa ladha mashabiki. Baadhi ya nyota wa zamani katika soka wakiwemo Pele, Zinedine Zidane na Lothar Matthaeus watakuwepo kusaidia uapngwaji ratiba hiyo wakati maofisa 5,000, waandishi wa habari na wageni waalikwa watakuwa wakishuhudia tukio hilo muhimu. Brazil imesubiri kwa miaka 64 kuandaa michuano hiyo baada ya kushindwa kunyakuwa kombe hilo mwaka 1950 katika mchezo wa fainali dhidi ya majirani zao Uruguay katika Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro.
No comments:
Post a Comment