Wednesday, January 1, 2014

ALLEGRI AHOFIA KIBARUA CHAKE MILAN.

MENEJA wa klabu ya AC Milan, Massimiliano Allegri amekiri kuwa 2013 itakuwa ndio Christmas yake ya mwisho akiwa hapo lakini amepania kuiwezesha timu hiyo kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya. Allegri alichukua mikoba ya kuinoa timu hiyo mwaka 2010 na kufanikiwa kushinda taji la Serie A katika msimu wake wa kwanza lakini toka kipindi hicho timu hiyo imekuwa ikisuasua katika ligi na michuano ya Ulaya. Kwa sasa Milan wako nyuma kwa alama 17 na timu inayoshika nafasi ya tatu lakini Allegri ana uhakika kuwa timu hiyo inaweza kupambana na kuhakikisha inamaliza katika nafasi za juu. Allegri amesema anatamani wazo la kumaliza mkataba wake wa miaka minne lakini anadhani itakuwa ni mingi sana kukaa kwenye klabu moja.


No comments:

Post a Comment