Wednesday, January 1, 2014

OBI MIKEL, DROGBA, YAYA TOURE KUCHUANA KATIKA TUZO ZA MWANASOKA WA MWAKA WA AFRIKA.

KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Nigeria, John Obi Mikel amefanikiwa kuwemo katika orodha ya mwisho ya wachezaji watatu wanaogombea tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka 2013 barani Afrika. Shirikisho la Soka la Afrika-CAF lilitangaza orodha yake ya mwisho jana ya wachezaji watakaogombea tuzo ambapo mbali na Obi Mikel pia wamo nyota wawili kutoka Ivory Coast ambao ni Yaya Toure na Didier Drogba. Hiyo inakuwa ni mara ya pili mfululizo kwa Toure na Drogba kuingia katika hatua hiyo ambapo mshindi anatarajiwa kutangazwa januari 9 katika sherehe zitakazofanyika jijini Lagos Nigeria. Kwa upande wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya bara hilo orodha ya mwisho ya wachezaji watatu ni Ahmed Fathy na Mohamed Abou Trika wote wa Misri ambao wako sambamba na Sunday Mba kutoka Nigeria. Toure ndiye anayeshikilia tuzo hiyo kwasasa kwa upande wa wachezaji wanaocheza nje ya Afrika wakati Abou Trika yeye anashikilia tuzo ya wachezaji wa ndani.

No comments:

Post a Comment