Thursday, January 2, 2014

BARCELONA YAMNYATIA LUIZ KWA MARA NYINGINE.

KLABU ya Barcelona imeanza kujaribu tena uwezekano wa kumsajili beki wa Chelsea David Luiz. Tayari kuna tetesi kuwa maofisa wa Barcelona wameshafanya mawasiliano na Chelsea kuhusu nyota huyo wa kimataifa wa Brazil muda mfupi baada ya Christmas huku beki huyo naye akitaka kuondoka katika timu hiyo. Chelsea wako tayari kusikiliza ofa rasmi watakayotoa Barcelona kwa beki huyo mwenye umri wa miaka 26 lakini Jose Mourinho anamchukulia Luiz kama rasilimali muhimu na atakubali kumuachia kama likitolewa fungu la kutosha. Akihojiwa Septemba mwaka jana Luiz amesema Barcelona alitoa ofa ya kumsajili lakini aliamua kubakia Chelsea huku Mourinho naye akidai bado anamhitaji beki huyo kusaidia na John Terry katika safu yake ya ulinzi.

No comments:

Post a Comment