KLABU ya Chelsea imethibitisha kuwa kiungo Frank Lampard na beki Branislav Ivanovic wanatarajiwa kukaa nje ya uwanja mpaka mwishoni mwa mwezi huu. Kufuatia ushindi wa mabao 3-0 waliopata dhidi ya Southampton ambao umewaacha wakiwa nyuma ya vinara wa ligi Arsenal kwa alama mbili, Jose Mourinho amesema majeruhi waliyopata wachezaji hao katika mchezo dhidi ya Liverpool utawaweka nje kwa mwezi mzima. Ivanovic ambaye ni raia wa Serbia alitlewa nje katika kipindi cha kwanza katika mchezo huo baada ya kuumia goti wakati Lampard alipata majeruhi ya msuli na kushindwa kurejea uwanjani baada ya kipindi cha mapumziko. Nyota hao wanatarajiwa kukosa mchezo wa mzunguko wa tatu wa Kombe la FA dhidi ya Derby County kabla ya timu hiyo haijakwaana na Hull City, Manchester United na West Ham United baadae mwezi huu.
No comments:
Post a Comment