Thursday, January 2, 2014

FABREGAS AMTABIRIA MAKUBWA MESSI.

KIUNGO wa klabu ya Barcelona, Cesc Fabregas ametabiri kuwa mchezaji mwenzake Lionel Messi anakuwa kama mbogo aliyejeruhiwa wakati atakaporejea baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili kutokana na majeraha ya msuli. Messi alirejea tena Barcelona jana akitokea kwao Argentina ambako alimaliza matibabu yake na anatarajia kujiunga na Fabregas pamoja na kikosi kizima cha Gerardo Martino katika mazoezi. Martino anatarajia kutokuwa na haraka ya kumpanga katika kikosi chake cha kwanza Messi lakini kuna uwezekano wa kumpa muda kidogo wa kucheza katika mechi dhidi ya Elche mwishoni mwa wiki hii. Fabregas amesema Messi alihitaji mapumziko aliyopata haswa ikizingatiwa tatizo lililokuwa likimsumbua limekuwa likijiridia hivyo kulikuwa hakuna jinsi zaidi ya kusimama kucheza.

No comments:

Post a Comment