KLABU ya Cardiff City imethibitisha kumteua Ole Gunner Solskjaer kuwa meneja mpya wa klabu hiyo. Solskjaer anachukua nafasi ya mikoba ya Malky Mackay ambaye alitimuliwa na mmiliki wa klabu hiyo ya Wales Vincent Tan. Toka kutimuliwa kwa Mackay, David Kerslake ndiye aliyepewa mikoba ya muda ya kuinoa klabu hiyo na kuingoza kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Sunderland na baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Arsenal. Akihojiwa mara baada ya uteuzi huo Solskjaer ambaye alikuwa mshambuliaji wa zamani wa Manchester United amesema hiyo ni changamoto mpya kwake na anategemea kuisaidia Cardiff kupiga hatua nyingine.
Thursday, January 2, 2014
CARDIFF SASA KUNOLEWA NA JEMBE LA ZAMANI LA MAN UNITED.
KLABU ya Cardiff City imethibitisha kumteua Ole Gunner Solskjaer kuwa meneja mpya wa klabu hiyo. Solskjaer anachukua nafasi ya mikoba ya Malky Mackay ambaye alitimuliwa na mmiliki wa klabu hiyo ya Wales Vincent Tan. Toka kutimuliwa kwa Mackay, David Kerslake ndiye aliyepewa mikoba ya muda ya kuinoa klabu hiyo na kuingoza kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Sunderland na baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Arsenal. Akihojiwa mara baada ya uteuzi huo Solskjaer ambaye alikuwa mshambuliaji wa zamani wa Manchester United amesema hiyo ni changamoto mpya kwake na anategemea kuisaidia Cardiff kupiga hatua nyingine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment