Monday, January 6, 2014

BLATTER ACHUKIZWA NA BRAZIL KUCHELEWESHA MAANDALIZI YA KOMBE LA DUNIA.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter ameonyesha kutofurahishwa kwake na jinsi Brazil wanavyofanya maandalizi ya taratibu kwa ajili ya Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika Juni mwaka huu. Akihojiwa Blatter amesema nchi hiyo imekuja kutambua kuwa walianza maandalizi wakiwa wamechelewa ndio mpaka sasa hawajamaliza ujenzi wa baadhi ya viwanja. Blatter amesema Brazil ni nchi pekee iliyochelewesha maandalizi yake kwa ajili ya michuano hiyo toka achukue madaraka ya kuiongoza FIFA pamoja na kuwa na miaka saba ya kujiandaa. Rais huyo pia aliwaondoa hofu ya uwezekano wa maandano katika michuano hiyo kama ilivyotokea katika michuano ya Kombe la Shirikisho Juni mwaka jana. Blatter amesema mchezo wa soka utalindwa na anaamini wananchi wa Brazil hawatashambulia mchezo huo moja kwa moja kwasababu soka katika nchi hiyo ni kama dini kwa jinsi unavyopendwa. Kombe la Dunia linatarajiwa kuanza rasmi kutimua vumbi Juni 12 huku mchezo wa fainali ukitarajiwa kuchezwa Julai 13.

No comments:

Post a Comment