SHIRIKISHO la Soka Duniani, FIFA limekihoji Chama cha Soka nchini Misri, EFA kuhusu tuhuma kutoka katika vilabu vingi nchini humo wakilalamikia serikali kuingilia masuala ya michezo hususani soka. Vilabu vingi kama Al Ahly, Zamalek na El Tram vyote vimelalamika hadharani kuhusu serikali kuingilia mambo ya soka. Hatua hiyo imekuja kufuatia waziri wa michezo wan chi hiyo Taher Abu Zaied kufunja bodi ya ya Zamalek miezi michache iliyopita na kutaka kufanya hivyo tena katika bodi ya Al Ahly wiki iliyopita. FIFA imeitaka EFA kushughulikia tatizo hilo mapema kabla ya Februari 5 mwaka huu jambo ambao maofisa wa shirikisho hilo wameahidi kuzungumza na vilabu ili kutatua tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment