MADAKTARI wanaomtibu dereva nyota wa mbio za langalanga kutoka Ujerumani, Michael Schumacher wamedai kuwa hali yake imetengemaa kidogo baada ya kufanyiwa upasuaji wa pili ili kupunguza msukumo katika ubongo. Dereva huyo ambaye ni bingwa wa dunia mara saba wa mashindano ya langalanga alipata majeraha ya kichwa katika ajali aliyopata wakati akiteleza katika barafu katika milima ya Ufaransa. Schumacher mwenye umri wa miaka 44 bado amebakia katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu kwa siku ya tatu leo kwenye hospitali ya Chuo Kikuu cha Grenoble. Madaktari wake wamesema pamoja na hali yake kutengemaa kidogo lakini bado hajaondoka katika hatari ya kupoteza maisha.
No comments:
Post a Comment