MENEJA wa klabu ya Manchester United, David Moyes amemkosoa mwamuzi Howard Webb kwa kutotoa penati kwa timu yake baada ya kipigo cha mabao 2-1 walichopata kutoka Tottenham Hotspurs. Kauli ya Moyes imekuja kufuatia golikipa wa Spurs Hugo Lloris kumuangusha katika eneo la hatari Ashley Young katika dakika ya 87 ambapo Webb alikataa kutoa penati. Moyes amesema kuwa ilikuwa ni penati ya wazi na kama hawakupewa hafikiri kwamba wanaweza kupata nyingine katika msimu huu wa Ligi Kuu. Mbali na Moyes lakini pia kocha wa Spurs Tim Sherwood naye aliunga mkono kwamba ilikuwa ni penati lakini anashukuru mwamuzi hakuliona tukio kwa karibu na kuwawezesha kuondoka na alama zote tatu.
No comments:
Post a Comment