KLABU ya Real Madrid imetajwa kuwa klabu iliyoingiza mapato mengi zaidi katika msimu wa 2012-2013 na kuongeza rekodi yao ya kushikilia nafasi hiyo kwa misimu tisa mfululizo. Kwa mujibu wa takwimu hizo zinazotolewa na Deloitte Football Money League klabu hiyo ya Hispania imeingiza kiasi cha euro milioni 518.9 na kuwazidi mahasimu wao Barcelona kwa euro milioni 36.3. Klabu ya Manchester United ambayo imewahi kuongoza katika orodha hiyo msimu wa 1996-1997 na 2003-2004 imedondoka katika nafasi tatu za juu kwa mara ya kwanza na nafasi yao kuchukuliwa na mabingwa wa ulaya Bayern Munich ambao wamewazidi United kwa euro milioni 7.4. Klabu ya Paris Saint-Germain,PSG ya Ufaransa imekwea mpaka nafasi ya tano katika orodha hizo kutoka nafasi ya 10 waliyokuwepo baada ya kufanikiwa kuongeza mapato yao kwa asilimia 81. Orodha kamili ya vilabu 10 vinavyoingiza mapato zaidi nia kama ifuatayo, Madrid euro milioni 518.9, Barcelona euro milioni 482.6, Bayern Munich euro milioni 431.2, Manchester United euro milioni 423.8, PSG euro milioni 398.8, Manchester City euro milioni 316.2. Nyingine ni Chelsea euro milioni 303.4, Arsenal euro milioni 284.3, Juventus euro milioni 272.4 na AC Milan ndio wanafunga orodha ya kumi bora wakiingiza mapato yanayofikia euro milioni 263.5.
No comments:
Post a Comment