MENEJA wa klabu ya Barcelona, Gerardo Martino amesisitiza kuwa hataharakisha kumchezesha Lionel Messi katika mchezo wa La Liga dhidi ya Atletico Madrid mwishoni mwa wiki hii. Messi hajacheza mechi yoyote toka achanike msuli katika mchezo dhidi Real Betis Novemba mwaka jana na alitazama akiwa jukwaani mchezo dhidi ya Elche jana ambao Barcelona ilishinda kwa mabao 4-0 na kuwarejesha kileleni mwa msimamo wa La Liga. Hata hivyo, Messi tayari ameanza mazoezi na kuna uwezekano akapangwa katika mechi ya Kombe la Mfalme dhidi ya dhidi ya Getafe Jumatano au mcezo dhidi ya Atletico siku tatu baadae. Pamoja na tetesi hizo Martino amesema hana haraka ya kumpanga nyota huyo mpaka atakapojiridhisha kwamba yuko fiti kimwili na kiakili.
No comments:
Post a Comment