Tuesday, February 11, 2014

AFRIKA KUSINI YATAKA KUANDAA MICHUANO YA JUMUIYA YA MADOLA 2022.

SERIKALI ya Afrika Kusini inafikiria kutuma maombi kwa ajili ya kuandaa michuano ya Jumauiya ya Madola mwaka 2022. Rais wa Kamati ya Olimpiki nchini humo Gideon Sam ana mategemeo ya kuileta michuano hiyo katika bara la Afrika kwa mara kwanza kwasababu anadhani wakati wake umefika. Msemaji wa kitengo cha habari katika wizara ya michezo ya nchi hiyo amesema waziri Fikile Mbalula tayari amepokea maombi hayo na amakubali. Akihojiwa Sam amesema anadhani Afrika iko tayari kwa ajili ya michuano hiyo na Afrika Kusini inaweza kuandaa michuano hiyo kwa urahisi kwasababu tayari kuna miundo mbinu baada ya kuandaa mashindano mbalimbali ya kimataifa. Wizara ya michezo sasa itafanya kazi pamoja na kamati hiyo kabla ya kuwasilisha katika Baraza la Mawaziri nchini humo kwa uamuzi wa mwisho.

No comments:

Post a Comment