Monday, February 3, 2014

ANCELOTTI AMKOSOA MWAMUZI KUHUSU KADI NYEKUNDU YA RONALDO.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amekosoa uamuzi uliotolewa na mwamuzi Miguel Ayza wa kumpatia Cristiano Ronaldo kadi nyekundi ya moja kwa moja wakati timu hiyo ikitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Athletic Bilbao jana usiku. Ronaldo alitolewa nje baada ya mabishano kati yake na wachezaji wa Bilbao, Carlos Gurpegui na Ander Iturraspe katika dakika ya 76 ya mchezo lakini Ancelotti anadhani nyota huyo wa kimataifa wa Ureno hakustahili kutolewa kwa tukio hilo. Akihojiwa Ancelotti amesema ni ngumu kwake kusema kwasababu hakuwa karibu na eneo la tukio lakini picha zinaonyesha kuwa tukio hilo halikuwa baya kiasi cha kutoka kadi nyekundu. Ancelotti pia alikiri kuwa kadi nyekundu kwa Ronaldo ilisababisha kikosi chake kipate wakati mgumu lakini ameridhishwa na matokeo ya sare waliyopata pamoja na kushindwa kuwapita mahasimu wao Barcelona waliochapwa mabao 3-2 na Valencia Jumamosi. Kwasasa Madrid wako katika nafasi ya tatu katika msimamo wa La Liga wakipitwa kwa alama tatu na vinara Atletico Madrid.

No comments:

Post a Comment