Tuesday, February 18, 2014

COLE HATIHATI KUCHEZA KOMBE LA DUNIA.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amezusha wasiwasi juu ya mustakabali wa Ashley Cole kuitwa katika timu ya taifa ya Uingereza kwa kukataa kuthibitisha kama atampa muda wa kucheza beki huyo. Mkataba wa Cole unamalizika mwishoni mwa msimu huu na nyota huyo anaonekana kupoteza namba yake katika kikosi cha kwanza kwa Cesar Azpilicueta. Beki huyo mwenye umri wa miaka 33 pia anaonekana kuwa katika mapambano ya kuingia katika kikosi cha Uingereza kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu. Akiulizwa kama atampa Cole muda wa kucheza, Mourinho hajajua mpaka sasa kwani anafuraha kwa jinsi Azpilicueta anavyocheza vizuri katika nafasi hiyo. Cole hajaanza kucheza katika kikosi cha kwanza cha Chelsea toka mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Hull City Januari 11 na pia hakuwemo katika kikosi kilichong’olewa katika Kombe la FA na Manchester City Jumamosi iliyopita hivyo kuzusha tetesi kuwa beki huyo anaweza kuondoka katika majira ya kiangazi. Mourinho amesema hawezi kufikiria kuhusu timu za taifa wakati huohuo akafikiria timu yake ndio maana kunakuwa na makocha wa timu hizo hivyo haijalishi kama mchezaji anacheza katika klabu kwasababu huwa nao wanachagua wachezaji wanaowafaa.

No comments:

Post a Comment