KIUNGO wa zamani wa klabu ya Bayern Munich, Paul Breitner anaamini kuwa wachezaji watatu wa timu hiyo Philipp Lahm, Manuel Neuer na Franck Ribery wana namba za kudumu katika kikosi cha kwanza. Mustakabali wa Toni Kroos na Mario Mandzukic ambao wote walikuwa sehemu muhimu katika mataji matatu Bayern waliyoshinda, umekuwa shakani kwa wiki za karibuni kutokana na Kroos kushindwa kuafikiana juu mkataba mpya huku Mandzukic akienguliwa katika kikosi cha kwanza. Breitner anaamini kuwa Bayern wana kikosi imara hata kama wakiwakosa wachezaji hao wawili na Ribery ambaye atakosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal kutokana na majeruhi hawezi kuathiri sana kikosi cha timu hiyo kinachonolewa na Pep Guardiola. Kiungo huyo amesema Bayern sio kwamba wana timu bora duniani kwasasa bali pia wana kikosi bora kabisa duniani. Breitner aliendelea kudai kuwa kila mchezo katika kikosi hicho anaweza kubadilishwa kasoro wachezaji watu ambao ni Neuer, Ribery na Lahm.
No comments:
Post a Comment