NYOTA wa zamani wa tenisi kw upande wa wanaume Pete Sampras wa Marekani anaamini kuwa Roger Federer wa Switzerland bado ana uwezo na kasi ya kuweka rekodi ya kunyakuwa taji la michuano ya Wimbledon kwa mara ya nane. Sampras na Federer wote kwa pamoja wamewahi kushinda taji hilo mara saba kila mmoja. Lakini taji la mwisho kubwa kwa Federer mwenye umri wa miaka 32 lilikuwa la Wimbledon alilonyakuwa mwaka 2012. Kutokana na kiwango kibovu alichoonyesha mwaka jana kumepelekea baadhi ya wadau wa mchezo huo kudai kuwa nyota huyo mwenye rekodi ya kunyakuwa mataji 17 kuwa amekwisha makali yake. Hata hivyo Sampras mwenye umri wa miaka 42 hivi sasa amesema bado ni mapema sana kumuondoa Federer kwani kama akiendelea kufurahia na kuwa na afya anaweza kucheza kwa miaka mingine miwili zaidi au minne.
No comments:
Post a Comment