MENEJA wa klabu ya Barcelona, Gerardo Martino amesisitiza kuwa hana wasiwasi na suala la Lionel Messi kushindwa kufunga mabao. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina amefunga bao moja toka mwezi Octoba mwaka jana na alishindwa tena kufunga katika mechi waliyoibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Real Sociedad jana usiku. Hata hivyo Martino amesema anafurahi na jinsi nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 anavyotengeneza nafasi za kufunga wakati wa mechi na shaka kwamba atarejesha makali yake siku si nyingi. Kocha huyo aliendelea kusema hatishwi na ukame wa mabao alionao kitu cha muhimu ni kusaidia timu kushinda kwasababu huwa hacheza peke yake uwanjani.
No comments:
Post a Comment