KLABU ya Valencia ya Hispania imetangaza kumsajili beki wa FC Porto Nicolas Otamendi kwa ada ya paundi milioni 12 huku wakimpa mkataba wa miaka mitano. Beki huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye atajiunga na klabu hiyo Julai mwaka huu amekuwa akiwindwa na vilabu mbalimbali vikubwa barani Ulaya wakiwemo Manchester United, Manchester City na Monaco. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina amejiunga na Valencia kufuata nyayo za nyota wengine wa nchi hiyo waliopo hapo kama Mario Kempes, Roberto Ayala na Pablo Aimar. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Otamendi amesema baada ya kucheza kwa kipindi kirefu Porto ni heshima kubwa kwake kujiunga na klabu kama Valencia katika hatua hii nyingine katika maisha yake ya soka. Otamendi amesema atafanya kila analoweza ili kuhakikisha anacheza kwa mafanikio kwenye klabu hiyo yenye historia ya kipekee.
No comments:
Post a Comment