KOCHA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya Uingereza, baada ya timu hiyo kuweka rekodi nzuri Januari ikishinda mechi nne kati ya nne. Huu ni mwezi wa pili mfululizo Pellegrini anashinda tuzo hiyo na mara ya kwanza kwa kocha mmoja kushinda mara mbili mfululizo tangu Carlo Ancelotti afanye hivyo akiwa kocha wa Chelsea mwaka 2011. Nyota wa Sunderland, Adam Johnson ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu baada ya kazi nzuri aliyoifanya mwezi uliopita akifunga mabao matano. Johnson amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Sunderland akiisaidia kutoka mkiano mwa msimamo wa ligi huku akifunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 4-1 waliopata kutoka kwa Fulham.
No comments:
Post a Comment