Saturday, February 8, 2014

RANIERI AIGWAYA PSG.

MENEJA wa klabu ya Monaco, Claudio Ranieri aedai kuwa hatajalisha kama timu hiyo itafungwa katika uwanja wake wa nyumbani na Paris Saint-Germain, PSG katika mchezo baina timu hizo utakaochezwa kesho. Monaco ambao wamepanda daraja msimu uliopita wamezidiwa alama tano na PSG katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Ufaransa, wamefanya usajili wa majina makubwa msimu huu ili kuimarisha kikosi chao akiwemo Dimitar Berbatov ambaye wamemchukua Januari hii. Ranieri amesema kwao mechi dhidi ya PSG ni kama mchezo wa kirafiki, watajitahidi kushinda lakini wanatakiwa kukubali ukweli. Kocha huyo aliendelea kusema kuwa PSG wameshamaliza kujenga kikosi chao na wao bado wanajipanga kujenga cha kwao hivyo hiyo ndio tofauti kubwa waliyonayo kwa timu hizo. Ranieri amesema kama wakishindwa kuwafunga PSG watakuwa nyuma yao kwa alama nane lakini haijalishi kwsababu hawana mpango wa kutaka kunyakuwa taji la ligi msimu huu.

No comments:

Post a Comment