MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa klabu hiyo imefikia makubaliano ya mkataba mpya na Tomas Rosicky. Novemba mwaka jana kulizuka tetesi kuwa kiungo huyo atapewa mkataba mpya kama akifanikiwa kucheza mechi 25 za klabu hiyo msimu huu. Risicky alicheza mechi yake ya 26 wakati Arsenal ikiibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Sunderland JUmamosi iliyopita na Wenger hana kwamba anahitaji kumbakisha nyota huyo mwenye umri wa miaka 33. Akihojiwa Wenger amesema Rosicky atabakia na tayari wameshafanya mazungumzo ambayo yatawekwa wazi mapema iwezekanavyo. Rosicky alirejea katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo na kufunga bao wakati Mesut Ozil alipopumzishwa.
No comments:
Post a Comment