Friday, March 7, 2014

BARCELONA YAMNYAKUWA KIPA WA BORUSSIA MONCHENGLADBACH.

KUNA tetesi kuwa klabu ya Barcelona imefikia makubaliano na timu ya Borussia Monchengladbach juu ya uhamisho wa Marc-Andre ter Stegen kwa ada ya kati ya euro milioni 9 na 12 pamoja na mechi mbili za kirafiki baina ya timu hizo. Barcelona wamekuwa sokoni kutafuta golikipa kufuatia kuondoka kwa Victor Valdes mwishoni mwa msimu huu na sasa wanaonekana tayari wamemnasa Ter Stegen. Kipa huyo wa kimataifa wa Ujerumani anatarajiwa kusaini mpaka mkapa majira ya kiangazi mwaka 2019 na Barcelona. Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Andoni Zubizarreta amekuwa akisafiri kwenda Ujerumani mara nyingi katika miezi michache iliyopita ili kumfuatilia golikipa huyo akicheza na ameonekena kuridhika na kiwango chake. Golikipa huyo mwenye umri wa miaka 21 alitangaza kutoongeza mkataba na klabu hiyo ambao unaishia mwaka 2015 hivyo Monchengladbach watalazimika kumuuza kiangazi.

No comments:

Post a Comment