Friday, March 7, 2014

PARDEW AOMBA SHAURI LAKE KUSIKILIZWA FARAGHA.

MENEJA wa klabu ya Newcastle United, Alan Pardew amekiri kushitakiwa kwa makosa ya utovu wa nidhamu na Chama cha Soka nchini Uingereza, FAkufuatia kumpiga kichwa mchezaji David Meyler wa Hull City wakati wa mechi ya Ligi Kuu baina ya timu hizo mwishoni mwa wiki iliyopita. Pardew ambaye ametozwa faini ya paundi 100,000 na klabu yake ameomba FA kusikiliza kesi yake faragha. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 ambaye pia amewahi kuzinoa West Ham United na Southampton tayari ameomba radhi kwa tukio hilo lakini anategemewa kupewa adhabu ya kufungiwa mechi nyingi. Hiyo sio mara ya kwanza kwa Pardew kujikuta mbele ya jopo la kamati ya nidhamu ya FA kwnai Septemba mwaka 2012 alitozwa faini ya paundi 20,000 na kufungiwa mechi mbili kwa kumsukuma mwamuzi msaidizi Peter Kirkup wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya Tottenham Hotspurs.

No comments:

Post a Comment