MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ameshitakiwa na Chama cha Soka cha Uingereza, kwa tabia zisizo za kiungwana baada ya kuondolewa katika benchi lake la ufundi katika mchezo dhidi ya Aston Villa Jumamosi iliyopita. Mashitaka hayo yanahusiana na Mourinho kuingia uwanjani na kuzungumza na mwamuzi Chris Foy kufuatiwa kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kiungo wake Ramires. Mapema katika mchezo huo Willian pia alipewa alitolewa nje. FA imempa Mourinho mpaka Jumatatu kuwa amejibu mashtaka hayo. Ramires alipewa kadi ya moja kwa moja katika mchezo huo baada ya kumuingilia vibaya kwa miguu miwili mchezaji wa Villa Karim El Ahmadi.
No comments:
Post a Comment