Friday, March 7, 2014

HALI YA SCHUMACHER BADO TETE.

MADAKTARI wanaomtibu nguli wa mashindano ya langalanga Michael Schumacher badp wanapambana ili kujaribu kumuondoa dereva huyo katika dozi ya usingizi mzito waliyompa. Dereva huyo bingwa mara saba wa dunia mwenye umri wa miaka 45 alipata majeraha ya kichwa wakati akiteleza katika barafu katika milima ya Ufaransa Desemba 29 mwaka jana. Akihojiwa meneja wa Schumacher, Sabine Kehm amesema madaktari bado wanajaribu kumuondolea dozi ya usingizi taratibu na hali haijabadilika. Madaktari walimweka katika dozi nzito ya usingizi dereva huyo ili ubongo wake uweze kupata nafasi ya kupona taratibu baada ya kufanyiwa upasuaji mara mbili kutokana na ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment