Friday, March 7, 2014

PSG YAKUTANA NA JUVENTUS KUZUNGUMZIA UHAMISHO WA POGBA.

RAIS wa klabu ya Paris Saint-Germain,PSG Nasser Al-Khelaifi amekutana na mwenzake wa Juventus Andrea Agnelli katika hoteli ya Paris kuzungumzia uhamisho wa Paul Pogba. Kwa kipindi kirefu PSG wamekuwa wakihusishwa na kumtaka nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa ili kuongeza nguvu katika kikosi chao katika majira ya kiangazi yanayokuja na Al-Khelaifi ameamua kutupa karata yake ya kwanza kwa ajili ya Pogba. Pogba kwa sasa ana mkataba na Juventus mpaka majira ya kiangazi mwaka 2016 na mabingwa hao Serie A wanataka kubakiza nyota huyo zaidi ya mmkataba wake utakapomalizika. Hata hivyo Agnelli amekiri mapema wiki hii kuwa hata kama hawana nia ya kumuuza kiungo huyo mwenye nguvu klabu hiyo haina uwezo wa kumzuia kama fungu kubwa litatoka kwa ajili yake.

No comments:

Post a Comment