WANG’AMUZI vipaji 28 wanatarajiwa kukutana Lushoto mkoani Tanga kwa siku saba katika mpango maalumu wa maboresho ya Taifa Stars ambapo watatoka na orodha ya mwisho ya wachezaji waliopatikana katika mechi za maboresho hayo zilizochezwa nchi nzima. Katika kikao hicho, wang’amuzi hao watapitia majina ya wachezaji walioteuliwa ikiwemo kuwaangalia tena kwenye video kwa vile mechi zote zilirekodiwa. Wachezaji watakaoteuliwa katika mpango huo baadaye wataingia kambini mkoani Mbeya. Wakati huo huo Bodi ya Ligi Kuu Tanzania-TPLB imeipiga faini ya jumla ya sh. milioni moja klabu ya Simba kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo vitendo vinavyoashiria ushirikina uwanjani. Simba ilifanya vitendo hivyo katika mechi yake dhidi ya Mbeya City ambapo imepigwa faini ya sh. 500,000 huku wakipigwa faini nyingine ya 500,000 kwa makocha wake Zdravko Logarusic, Selemani Matola na Idd Pazi kuingia uwanjani na kumzonga mwamuzi kwenye mechi hiyo.

No comments:
Post a Comment