MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa Mesut Ozil atang’ara wakati timu hiyo itakapoikabili Bayern Munich katika mchezo wa mkondo wa pili wa michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kesho. Kikosi cha Wenger kitasafiri kwenda nchini Ujerumani kwa ajili ya mchezo wao wa Jumanne huku wakiwa nyuma kwa mabao 2-0 waliyofungwa katika mchezo wa kwanza lakini watakwenda wakijiamini kwa kuwa na kumbukumbu ya kupata matokeo kama hayo katika Uwanja wa Alianz Arena msimu uliopita. Ozil alikosa penati katika mchezo wa kwanza uliochezwa katika Uwanja wa Emirates huku akicheza kwa kiwango cha chini lakini Wenger amesema nyota huyo amesahau tukio hilo na anarudi katika kiwango chake bora baada ya kufunga bao katika mchezo wa Kombe la FA walioshinda mabao 4-1 dhidi ya Everton. Wenger amesema anadhani Ozil amesharudi katika hali yake ya kawaida na hana shaka kwamba atacheza kwa kiwango cha juu katika mchezo dhidi ya Bayern.

No comments:
Post a Comment