Monday, March 10, 2014

NASRI AWAOMBA RADHI MASHABIKI WA CITYKWA KUNG'OLEWA FA.

KIUNGO mahiri wa klabu ya Manchester City, Samir Nasri amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo baada ya kutolewa katika michuano ya Kombe la FA na Wigan Athletic katika Uwanja wa Etihad. Kikosi cha Wigan kinachonolewa na Uwe Rosler mwaka jana kilifanikiwa kuifunga City katika hatua ya fainali ya michuano hiyo na wamerudia tena kufanya hivyo mwaka huu kwa kuitandika mabao 2-1 yaiyofungwa na Jordi Gomez na James Perch. Nasri amekiri kuwa kikosi cha City hakikucheza katika kiwango chake lakini amewataka wachezaji wenzake kuhamishia nguvu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Barcelona utakaochezwa Jumatano. Kiungo huyo aliendelea kuandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa kama kuna somo walilopata katika mchezo huo ni kila kitu kinawezekana katika soka hivyo hata wao wanaweza kubadilisha matokeo waliyopata dhidi ya Barcelona katika mchezo wa kwanza.

No comments:

Post a Comment