Monday, March 10, 2014

KIPIGO CHA WIGAN HAKIWEZI KUTUZUIA KUSHINDA MATAJI MENGINE - PELLEGRINI.

MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini amesema kipigo cha mabao 2-1 walichopata kutoka kwa Wigan Athletic hakitaleta madhara nafasi yao yakushinda mataji zaidi msimu huu. Mabingwa hao wa Kombe la Ligi hivi sasa wako nyuma ya vinara Ligi Kuu Chelsea kwa alama tisa huku wakiwa na mechi tatu mkononi. Pellegrini amesema tayari wameshashinda taji moja na bado wana mataji zaidi ya kupigania mpaka mwishoni mwa msimu huu. Kocha huyo amesema kwasasa wanahamishia nguvu zao katika mchezo dhidi ya Barcelona utakaochezwa Jumatano halafu watajaribu kukwea kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kushinda mechi zao tatu za mkononi walizonazo.

No comments:

Post a Comment