RAIS wa klabu ya Bayern Munich, Uli Hoeness leo amehudhuria mahakamani huko Bavarian kufuatia kuanza kusikilizwa kwa kesi yake. Hoeness anatuhumiwa kukwepa kulipa kodi katika fedha alizohifadhi huko Switzerland na anaweza kuhukumiwa kifungo kama akikutwa na hatia. Mwendesha mashitaka wa serikali Achim von Engel amedai kuwa Hoeness hakuonyesha kipato chake halisi ambacho kinafikia euro milioni 33 alizopata kati ya mwaka 2003 na 2009 hivyo kupelekea kukwepa kodi inayofikia euro milioni 3.5. Hoeness haraka alipeleka taarifa zake za fedha wakati aliposhitakiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2013 lakini mwendesha mashitaka alitupilia mbali nyaraka hizo na kudai kuwa haziko sawa na hazijakamilika.

No comments:
Post a Comment