MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuweka rekodi ya kuwa mshambuliaji mwenye mabao mengi zaidi kwa timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 5-1 waliopata dhidi ya Cameroon jana. Ronaldo hivi amefikisha mabao 49 kwa Ureno, mawili zaidi ya aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo Pauleta. Akihojiwa kuhusu rekodi hiyo, Ronaldo amesema hajali sana kuhusu mambo ya kuvunja rekodi kwasababu ni mambo ambayo huja yenyewe kama ukifanya kazi kwa bidii. Katika mchezo huo Ronaldo alifunga mabao yake katika dakika 21 na lingine katika dakika ya 83 huku mengine yakifunga na Raul Meireles dakika ya 65, Fabio Coentrao dakika ya 67 na Edinho dakika ya 77.
No comments:
Post a Comment