BEKI wa klabu ya Manchester City, Vincent Kompany amesema ushindi wa dakika za mwisho waliopata na kunyakuwa taji la Ligi Kuu 2012 ndio unaowapa matumaini kuelekea katika michezo yao minne iliyobakia. Ushindi wa mabao 3-1 iliyopata City dhidi ya West Bromwich Albion jana usiku umeifanya timu hiyo kupunguza pengo la alama na vinara Liverpool kufikia sita huku wakiwa wamebakiwa na mechi moja mkononi. City walinyakuwa taji lao la kwanza la ligi baada ya miaka 44 mwaka 2012, kwa mabao mwili yaliyofungwa katika dakika za majeruhi katika mechi ya mwisho wa msimu na Kompany ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo anaamini chochote kinaweza kutokea katika mechi zilizobakia. Kompany amesema hataki kukata tamaa kwasababu mwaka 2012 walitawadhwa mabingwa katika mchezo wa mwisho tena dakika za lala salama hivyo haoni kwanini hilo lishindikane safari kwasababu bado mechi nne kabla msimu haijamalizika.
No comments:
Post a Comment