MENEJA wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone ameonyesha kutokuwa na hofu na majeraha aliyopata Diego Costa katika mchezo dhidi ya Getafe ambao walishinda kwa mabao 2-0 jana usiku. Costa alilazimika kutolewa nje na machela katika dakika za mwishoni baada ya kujigonga katika nguzo ya goli wakati akiifungia bao la pili Atletico. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania aliubamiza mguu wake wa kushoto katika nguzo ya goli baada ya kumalizia pasi murua ya Adrian Lopez tukio ambalo lilimuacha na kidonda kikubwa katikati ya ugoko wake. Akihojiwa kuhusiana na tukio hilo, Simeone amesema nyota huyo hakuumia sana kwa ndani zaidi ya jeraha kubwa linaloonekana kwa nje.
No comments:
Post a Comment