SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetangaza kuwa Barcelona itaruhusiwa kusajili wachezaji katika kipindi cha usajili majira ya kiangazi baada ya kuamua kuisimamisha adhabu waliyopata kufuatia rufani waliyokata. Barcelona walikuwa wamefungiwa kufanya usajili kwa simu mmoja kutokana na kukiuka sheria za usjaili wa kimataifa kwa wachezaji walio na umri chini ya miaka 18 lakini adhabu hiyo imetenguliwa ikisubiri uamuzi wa mwisho katika rufani yao utakapotolewa. FIFA imefikia uamuzi huo baada ya kuona kuwa kamati yake ya rufani haiwezi kukutana katika kipindi hiki cha karibuni kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa Julai mosi mwaka huu. Uamuzi huo unamaanisha klabu hiyo inaweza kuendelea na taratibu zake za usajili majira ya kiangazi ikiwa tayari imeshamsajili kinga Alen Halilovic kutoka Dinamo Zagreb huku wakiwa mbioni kukamilisha usajili wa golikipa wa Borussia Monchengladbach Marc-Andre ter Stegen.
No comments:
Post a Comment