NGULI wa soka wa zamani wa Cameroon, Roger Milla amepoteza rekodi yake ya kuwa mchezaji mzee zaidi kuiwakilisha nchi yake barani Afrika kwa mshambuliaji wa Mauritius Kersely Appou mwenye umri wa miaka 43. Milla alijiwekea rekodi hiyo wakati alipofunga bao katika mchezo Cameroon waliofungwa na Urusi mabao 6-1 katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1994 akiwa na umri wa miaka 42 na siku 39. Bado anashikilia rekodi yake ya kuwa mchezaji mzee na kufunga bao katika michuano ya Kombe la Dunia. Appou alicheza katika kikosi cha Mauritius kilichofungwa na Mauritania katika mechi ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika Jumamosi iliyopita. Mshambuliaji ana umri wa miaka 43 na siku 354, umri ambao bado haujafikia wa mchezaji wa Visiwa vya Virgin McDonald Taylor anayeshikilia rekodi ya kwa kuwa mchezaji mzee zaidi kwa kucheza akiwa na umri wa miaka 46 na siku 217.
No comments:
Post a Comment