KLABU ya Manchester United kuna hati hati ya kumkosa mshambuliaji wake mahiri Wayne Rooney katika mchezo wa marudiano war obo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwasababu ya kuumia kidole gumba. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28 alipata maumivu hayo Jumanne iliyopita katika mchezo wa kwanza dhidi ya Bayern ambao walitoka sare ya bao 1-1. Meneja wa United, David Moyes amesema nyota huyo ameumia vibaya kidole gumba chake na inaweza kuwa tatizo katika mchezo wao dhidi ya Bayern. Hata hivyo Moyes amesema watajitahidi kumpa matibabu yote mwishoni mwa wiki na kuona kama anaweza kupona haraka kabla ya mchezo wao wa Jumatano ijayo.
No comments:
Post a Comment