Friday, April 4, 2014

SCHUMACHER AONYESHA DALILI NJEMA ZA KUZINDUKA.

WAKALA wa dereva nguli wa mashindano ya langalanga Michael Schumacher amedai kuwa mteja wake ameonyesha dalili za kuzinduka baada ya kupita miezi kadhaa akiwa hajitambui. Sabine Kehm amesema katika taarifa yake aliyotuma katika vyombo vya habari kuwa Schumacher ameonyesha dalili nzuri na kuongeza bado wana imani anaweza kuamka tena. Madaktari nchini Ufaransa wamekuwa wakifanya kazi kujaribu kumuondolea dozi nzito ya usingizi waliyompa ili aweze kuzinduka tena. Schumacher mwenye umri wa miaka 45 alipata majeraha makubwa kichwani katika ajali aliyopata wakati akiteleza katika barafu kwenye milima ya Ufaransa.

No comments:

Post a Comment