Friday, April 4, 2014

WACHEZAJI WA HISPANIA NAO WALISTAHILI BALLON D'OR KWA MAFANIKIO WALIYOPATA KIMATAIFA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque ameonyesha kusikitishwa kwake kwa kushindwa kutambulika kwa wachezaji wa Hispania kutokana na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kutawala tuzo za Ballon d’Or katika miaka ya karibuni. Ronaldo ameshinda tuzo hiyo mwaka 2008 na 2013 wakati Messi yeye amebeba tuzo hiyo kwa miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2009 mpaka 2012 huku wachezaji wa Hispania kama Xavi na Andres Iniesta wakizikosa. Hata hivyo Del Bosque anaamini kuwa mmoja kati ya wachezaji waliyoiongoza timu ya taifa ya Hispania kushinda taji la Ulaya 2008 na 2012 sambamba na Kombe la Dunia mwaka 2010 walitakiwa kushinda tuzo hiyo kwa mafanikio waliyopata. Kocha huyo amesema pamoja na kwamba hataki kumnyooshea mtu kidole lakini anadhani kuna wakati mmoja kati ya wachezaji wa Hispania alistahili kushinda tuzo ya Ballon d’Or.

No comments:

Post a Comment