KLABU ya Atletico Bilbao imejihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi mnono wa mabao 3-0 waliopata dhidi ya Rayo Vallecano jana usiku. Kikosi cha Bilbao kinachonolewa na Ernesto Valverde kilikuwa kinajua ushindi dhidi ya Vallecano ungewahakikishia nafasi katika michuano hiyo ikiwa ni mara ya kwanza toka walipofanya hivyo msimu wa 1997-1998 walipomaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga. Mabao ya Bilbao katika mchezo huo yalifungwa na Mikel San Jose, Oscar Marcos na Ander Herrer. Ushindi huo umeifanya Bilbao kuongeza pengo la alama baina yake na Sevilla kufikia tisa huku timu hiyo ikiwa na mechi tatu mkononi lakini hawataweza kuwafikia hata kama wakishinda mechi zote.
No comments:
Post a Comment