Saturday, May 3, 2014

GERRARD KUONGEZWA MKATABA LIVERPOOL.

MCHEZAJI mkongwe na nahodha wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard anatarajiwa kusaini mkataba mpya na timu hiyo ambao utamuweka hapo zaidi ya mwaka 2015. Nahodha huyo amebakiwa na miezi 12 katika mkataba wake wa sasa lakini bado amebakia katika mipango ya kocha Brendan Rodgers. Pamoja na kufanya makosa yalioipa mwanya Chelsea kushinda katika mchezo baina yao Jumapili iliyopita, Gerrard mwenye umri wa miaka 33 amekuwa nguzo muhimu kwa timu hiyo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu. Akihojiwa Rodgers amesema Gerrard atakuwa mchezaji mojawapo ambaye watamwongeza mkataba kwani bado yuko katika mipango yake huko mbele.

No comments:

Post a Comment