Saturday, May 3, 2014

FIFA YAMKATALIA FERNANDO KUICHEZEA URENO.

KIUNGO wa klabu ya FC Porto, Fernando amekataliwa nafasi ya kuichezea timu ya taifa ya Ureno baada ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kumkatalia maombi yake. Kiungo huyo mzaliwa wa Brazil alichukua uraia wa Ureno Desemba mwaka jana lakini aliwahi kuiwakilisha Brazil katika michuano ya vijana chini ya miaka 20 mwaka 2007. Ureno ilikuwa ikitegemea Diego Costa kukubali kuiwakilisha Hispania badala ya Brazil ingeweza kuwasaidia kupata kibali cha Fernando lakini FIFA wameweka wazi kuwa kiungo huyo ataruhusiwa kuchezea timu ya nchi aliyozaliwa pekee. Shirikisho la Soka Ureno lilipewa taarifa jana kuwa Fernando hataruhusiwa kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo kwa madai kuwa mchezaji huyo alikuwa hana uraia wa Ureno wakati akiiwakilisha timu ya vijana chini ya miaka 20 ya Brazil.

No comments:

Post a Comment