SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limethibitisha kuwa vilabu tisa vinatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina juu ya uwezekano wa kukiuka sheria za matumizi ya fedha. UEFA ilizifanyia uchunguzi vilabu 76 ambavyo viliombwa maelezo ya ziada ili kuhakiki kama hawakuvunja sheria hiyo katika msimu wa mwaka 2013-2014. Baada ya uchunguzi huo shirikisho hilo limechuja na kubakiwa na vilabu tisa ambavyo vitaendelea kuchunguzwa ingawa hawakuvitaja. Katika taarifa yao UEFA wamedai kuwa maelezo zaidi kuhusuaiana na suala yatatolewa pindi zoezi hilo litakapokamilika.
No comments:
Post a Comment