Wednesday, May 21, 2014

FALCAO KUJIUNGA NA WACHEZAJI WENZAKE WA COLOMBIA KATIKA KAMBI YAO NCHINI ARGENTINA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao anatarajiwa kusafiri na timu ya taifa ya nchi hiyo katika kambi yao waliyoweka nchini Argentina pamoja na taarifa kuwa nyota huyo anaweza kutitoa mwenyewe katika michuano ya Kombe la Dunia. Nyota huyo anayecheza klabu ya Monaco alipata majeruhi ya mabaya ya goti wakati wa mchezo wa Kombe la Ufaransa Januari mwaka huu na kumekuwa na madai kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekiri kushindwa kuwa fiti ili aweze kuiwakilisha nchi yake katika michuano hiyo nchini Brazil kiangazi hiki. Hata hivyo, kumetolewa taarifa na Shirikisho la Soka la Colombia wakibainihsa kuwa Falcao ambaye alifanya mazoezi na timu yake mwishoni mwa msimu bado anapambana ili kumuonesha kocha Jose Pekerman kwamba yuko fiti. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa Falcao atajiunga na wachezaji wenzake pindi watakaposafiri kwenda Buenos Aires na kwamba hivi sasa bado anafanya mazoezi ya viungo katika timu yake ya Monaco.

No comments:

Post a Comment