Wednesday, May 21, 2014

TOURE AZIDI KUWACHANGANYA MANCHESTER CITY.

KIUNGO mahiri Yaya Toure ameongeza tetesi za kuondoka Manchester City kwa kudai kuwa hajui timu gani ataichezea msimu ujao. Wakala wa mchezaji huyo, Dimitri Seluk alifafanua mapema kwamba nyota huyo anaweza kuondoka kwaababu anafikiri hatendewi haki na haeshimiwi na wamiliki wa timu hiyo. Sasa Toure mwenye umri wa miaka 31 amesema kila kitu kiko wazi kuhusu mustakabali wake katika siku zijazo. Akiulizwa kama anaweza kucheza katika klabu nyingine nyota huyo alikubali na kudai hawezi kujua kwasababu kila kitu kinawezekana katika soka. Toure aliendelea kudai kuwa kutokana na kuwa na msimu mzuri kila mtu anamzungumzia na wakala wake muda wote amekuwa katika simu na anajua nachotakiwa kufanya kwasababu anamwamini. Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast amesema kwasasa hawezi kujua yatakayotokea mbele lakini anataka kuhamishia mawazo yake katika michuano ya Kombe la Dunia na baada ya japo atajua cha kufanya huko. Toure amesaini mkataba mpya wa miaka minne na City Aprili mwaka jana.

No comments:

Post a Comment