Tuesday, May 6, 2014

HAMILTON ANAKARIBIA UBORA WAKE - MANSELL.

BINGWA wa zamani wa dunia wa mashindano ya langalanga, Nigel Mansell amedai kuwa dereva wa Marcedes Lewis Hamilton alikuwa anakribia ubora wake katika mashindano manne ya Grand Prix aliyoshindana mwaka huu. Hamilton raia wa Uingereza ambaye alishinda taji la dunia mwaka 2008, ameshinda mashindano matatu mfululizo baada ya kushindwa kumaliza mashindano ya ufunguzi ya Australi Grand Prix. Mansell mwenye umri wa miaka 60 amesema hakuna dereva yoyote aliyeshinda taji la dunia akiwa katika timu mbaya lakini kitu ambacho unaweza kufanya ni kuonyesha jinsi gani unaweza kushinda kutokana na kipaji ulichonacho jambo ambalo limefanywa na Hamilton msimu huu. Nguli huyo aliendelea kudai kuwa anadhani Hamilton anakaribia ubora wake kutokana na kuanza vyema mashindano ya langalanga msimu huu.

No comments:

Post a Comment